Malkia wa Nyuki akiwa na Alhaji Rage..
Tawi
maarufu zaidi la klabu ya Simba la Mpira Pesa, limerejea kundini na kutoa ahadi
ua ushirikiano mkubwa.
Mlezi wa
Simba, Rahma Al Kharusi ndiye amefanya kazi hiyo ya ziada ya kuzungumza na
viongozi wa tawi hilo jana jioni katika kikao kilichomalizika usiku.
Mama huyo
‘mwanajeshi’, maarufu kama Malkia wa Nyuki aliamua kuwarudisha wanachama hao
waliokuwa katika mgogoro mkubwa na Mwenyekiti, Ismail Aden Rage aliyetangaza
kulifuta.
Lakini
baada ya mazungumzo hayo, Mpira Pesa wanaojulikana kwa kuishangilia na kuipa
nguvu Simba walisema mambo yatakwenda vizuri na watarudi kushirikiana na
uongozi wa Simba kama ilivyokuwa awali ili kuisaidia katika mechi zilizobaki.
Malkia wa
Nyuki alifanya kikao hicho na kuwashawishi kurudisha ushirikiano ili kuunda
nguvu kubwa kwa Simba ambayo imegawanyika na kufanya iyumbe.
“Nashukuru
sana, kikao kimekwenda vizuri lakini watu wa Mpira Pesa wameonyesha ni waelewa
na wenye mapenzi makubwa na klabu yao. Wanaumizwa na matokeo mabaya.
“Nimewaomba
wakubali tushirikiane kuisaidia Simba katika wakati huu mgumu,
hawana tatizo na
hilo na ndilo jambo la msingi.
“Mambo
hayawezi kubadilika na kuwa mazuri kama tukiwa katika makundi, najua muda
unatakiwa lakini tukianza kwa kurudisha umoja, basi mambo yatakwenda vizuri tu,”
alisema Malkia wa Nyuki.
Malkia wa
Nyuki ndiye amekuwa jembe la kuiunganisha Simba ambayo imeyumba huku viongozi
wake wakianza kujiuzulu mfululizo ingawa Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage
amekuwa mgumu kama ‘nyundo’ kufanya hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment