Mchezaji wa zamani wa England, Paul Gascoigne anashikiliwa na jeshi la polis nchini humo kutokana na kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kumdhalilisha mpenzi wake.
Gascoigne maarufu kama Gazza ,46, alikamatwa baada ya kufanya vurugu katika kituo cha treni cha Hertfordshire, juzi usiku.
GAZZA AKIWA NA MKEWE (KUSHOTO KWAKE) NA FAMILIA YAKE KABLA YA KUTENGANE |
Polisi wa Hertfordshire walipigiwa simu na kuambiwa kuna mtu mlevi alikuwa anafanya vurugu katika eneo hilo.
Askari baada kufika katika eneo la tukio Gazza alipambana na polisi kwa kuwa hakutaka kuondoka eneo hilo.
Alimkaba koo mlinzi mmoja wa stesheni alipokuwa akijaribu kutaka kumuondoa katika eneo hilo.
Lakini hata mke wake waliyetengana aitwaye Sheryl Gascoigne alipojaribu kuingilia na kutaka kupoza mambo pia akamshambulia kwa maneno makali nay a kumdhalilisha.
Gazza alichukuliwa na kushikiliwa kituoni kwa saa 12 bila ya kufunguliwa mashitaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment