February 2, 2014


MPIRA UMEKWISHAAAAAA

Dk 82, Ngassa anapiga shuti kali nje ya 18 lakini linatoka nje

Dk 80, Kiiza anashindwa kufunga tena krosi nzuri ya Ngassa
Dk 76 Mbeya City wanamtoa Yeya, anaingia Saad Kipanga
Dk 75, Kiiza na kipa, baada ya kuutuliza mpira gamba, anashindwa kufunga

Dk 73, Yeya anaukosa mpira akiwa katika nafasi mfuli kufunga
Dk 70 Mbeya City wanamtoa Kaseke anaingia Joseph WilsonDk 68, Yanga wanaizidia Mbeya City kwa sana, shuti la Msuva linatoka kidogo nje ya lango

Dk 66, Ngassa anatoa krosi safi kwa Kiiza lakini anachelewa kuuguza mpira ujae wavuni
Dak 64 Yanga wanamtoa Kavumbagu anaingia Hamis Kiiza
Dk 63 Mbeya City wanamtoa Nonga anaingia Richard Peter


Dk 61, Yanga wanamtoa Twite anaingia Juma Abdul
Dk 56 Yanga wanafanya shambulizi kali,Msuva anashindwa kufunga akiwa na kipa

Dk 48, Luhende anapiga faulo, shuti kali linatoka sentimeta chache

Dk 46, Mazanda wa Mbeya City analambwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira kwa makusudi, ilikuwa ni kadi ya pili ya njano.
MAPUMZIKO
Dk 44, mashabiki Yanga wanamzomea Msuva baada ya kushindwa kuuwahi mpira


Dk 42, Nonga anapiga shuti tena linatoka pembeni kidogo
Dk 37, Msuva anawashanga mashabiki, baada ya kupata pasi akiwa mbele ya mabeki wa Mbeya City, anafunga breki na kurudisha mpira nyuma

Dk 35, Nonga anawatoka tena mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali lakini Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 29, Luhende akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga anashindwa kuitumia nafasi hiyo.


Dk 27, Magolo anamzidi ujanja Joshua na kupiga shuti linalopita sentimeta chache juu ya lango la Yanga.
Dk 24, krosi krosi ya Kaseke inatua kichwani kwa Nonga na mpira unatoka setimeta chache
Dk 18, Yanga wanafanya shambulizi tena lakini Msuva anaonekana kutokuwa makini...goal kick

GOOOOOOOOOO, Dk 15 Ngassa anaifungia Yanga bao baada ya kupiga shuti kali kwenye msitu wa mabeki wa Mbeya City
Dk 13, Matogolo anawatoka mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali, linatoka pembeni kidogo. Mbeya City wanaanza kucheza.


Dk 4, shuti kali la Luhende linamshinda kipa Mbeya City, lakini hakuna wa kumalizia, Yanga wanacheza pasi nyingi na kwa kujiamini zaidi


Dk 2 Yanga wanaingia tena, krosi safi ya Luhende inakosa mtu
Dk 1 Yanga wanafanya shambulizi, Kavumbagu anashindwa kuuwahi mpira

YANGA
Dida, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Cannavaro, Kelvin Yondani, Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa na David Luhende.

MBEYA CITY


David Burhan, Johh Kabanda, Hassan Mwasapila, Deo Julius, Yusuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga, Peter Mapunda na Deus Kaseke


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic