April 19, 2014


OLJORO

Rhino ya Tabora, Ashanti United na JKT Oljoro rasmi wameteremka daraja na kurejea Ligi Daraja la Kwanza.

Ashanti imeshuka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Prisons ya Mbeya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo.
ASHANTI UNITED

Wachezaji wa Ashanti United, walilia kwa uchungu wakionyesha kutofurahia kuteremka daraja.
Rhino nao wakiwa nyumbani Tabora, leo wamepigwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting. Hamis Mohammed na Elias Maguri ndiyo walioimaliza timu hiyo ya Tabora.
RHINO

Mjini Arusha, JKT OLjoro wameteremka rasmi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar. Timu hiyo ya jeshi inakuwa timu ya tatu kuteremka daraja.

Kutokana na kuteremka kwa timu hizo, Ndanda FC, Stand ya Shinyanga na Polisi ya Morogoro ndiyo wamepanda rasmi Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic