April 18, 2014


Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub  ‘Cannavaro’ amewaambia mashabiki na wapenzi wa timu yake kuwa, wasiwe na wasiwasi juu ya mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya  Simba kwa kudai kuwa kikosi chao kipo vizuri zaidi ya wapinzani wao hao na ana uhakika watashinda kwa mabao mengi.


Timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa ambapo mechi ya awali ya ligi hiyo matokeo yalisomeka 3-3, licha ya Yanga kuongoza kwa mabao 3-0 mpaka mapumziko.

Cannavaro amesema wachezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi mkubwa, licha ya kukosa ubingwa na kudai kuwa nia ni kulipa kile kipigo cha mabao 5-0 ambacho Yanga ilifungwa mwaka juzi.

Beki huyo mkongwe ameongeza kuwa, kipigo cha mabao matano walichokipata kipindi kile kimekuwa kikiwaumiza mpaka leo licha ya kuwa ni muda mrefu umepita.


“Kushinda mechi ya Jumamosi ndiyo kitu muhimu sana na lazima tulipize kipigo cha mabao matano ambayo tuliwahi kufungwa na watani wetu na nawaahidi mashabiki wetu tutawapa furaha baada ya kukosa ubingwa,” alisema Cannavaro kwa kujiamini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic