April 21, 2014





Kitendo kilichofanywa na wachezaji wa Yanga kuliondoa langoni na kulitupa kwa mashabiki taulo la kipa wa Simba, Ivo Mapunda, kimemkera kipa huyo na kufunguka wazi kuwa sababu kubwa iliyowafanya wachezaji hao kufanya hivyo ni kutokana na kuamini imani za kishirikina.

Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar timu hizo zilipokuwa zikiumana na matokeo kuwa sare ya kufungana bao 1-1.
Baada ya mpira uliopigwa na Msuva kuelekea langoni mwa Simba kuokolewa na Ivo ndipo Hamis Kiiza wa Yanga alikimbilia golini hapo na kuliondoa taulo hilo lililokuwa likining’inia kwenye nyavu za lango hilo na kulitupa chini kisha ndani ya nukta chache Didier Kavumbagu naye aliliokota na kwenda kulirusha kwa mashabiki ambao nao walilichanachana na kugawana vipandevipande.
Kocha wa makipa wa Simba, Idd Pazi, aliinuka mara moja akitokea kwenye benchi la ufundi la timu hiyo akiwa na taulo lingine mkononi na kulipeleka kwa kipa huyo ambaye naye akalining’niza nyavuni kwa mara nyingine, ndipo Mrisho Ngassa alilifuata na kulitoa tena na kuibua mtafaruku wa aina yake baina ya wachezaji wa timu hiyo lakini mwamuzi Dominic Nyamisana alilimaliza suala hilo na kumzawadia Kavumbagu kadi ya njano.

Dakika chache baadaye wakati mpira unaendelea, shabiki mmoja ambaye hakujulikana mara moja jina lake, aliruka uzio uwanjani hapo na kuliiba taulo hilo kisha kuwarushia tena mashabiki wa Yanga lakini baada ya tukio hilo, shabiki huyo alitiwa nguvuni na polisi waliokuwapo uwanjani hapo.
Mara baada ya mpira kumalizika, Ivo alisema: “Sijui ni kwa nini wachezaji wa Yanga waliamua kufanya hivyo, si kitendo cha kiungwana hata kidogo kuliondoa taulo langu na kulirusha kwa mashabiki, nafikiri walifanya hivyo wakiamini pengine lile taulo lina mambo ya kishirikina na hili nimekuwa nikilisikia mara kwa mara kutoka kwa watu mbalimbali kwamba lile taulo linahusishwa na imani za kishirikina kitu ambacho hakina ukweli wowote.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic