April 16, 2014


Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema anatamani mechi ya Simba na Yanga ipigwe usiku kwa kuwa ndiyo muda mzuri kwake.


Kocha huyo amesema kwa sasa ana furaha kubwa kwa kuwa jijini Dar es Salaam kuna hali ya baridi na mvua, lakini furaha yake itatimia kama mechi hiyo itapigwa usiku kwani ndiyo muda wake muafaka.

Mechi ya Yanga dhidi ya Simba inatarajiwa kupigwa Jumamosi hii majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Loga alisema anatamani mechi hiyo ingebadilishwa muda na ingekuwa usiku ingekuwa na faida kubwa sana kwake.

“Hii mechi ingepigwa usiku ingekuwa safi sana kwa sababu ingekuwa na faida nyingi, kwa watazamaji na hata kwangu pia; kwanza ingekuwa usiku wa saa moja hivi ingekuwa nafuu kwa wafanyakazi kupata muda wa kupumzika na kujiandaa kuja kwenye mechi.
“Najua hii mechi ni kubwa na kila mmoja angependa kuishuhudia na siku kama ya Jumamosi watu wengi wanaenda kazini na kufanya kazi kwa saa chache, hivyo ingewekwa usiku ingetoa muda mzuri kwa watu wote kuishuhudia.
“Halafu hata kwangu pia, ingekuwa safi kwani huwa napata shida muda wa mchana au jioni kutokana na kusikia sana joto na kutokwa jasho muda mwingi lakini hii hali ya hewa ya siku hizi mbili tatu imekuwa nzuri kwangu na hasa wakati wa usiku ndiyo huwa safi kabisa, natamani TFF waipeleke mechi hii ya Yanga na Simba wakati wa usiku.
“Kwa hiyo ingekuwa usiku mambo yangekuwa safi, lakini hili la usiku linawezekana kwa sababu uwanja una kila kitu kwa ajili ya giza, zipo taa kubwa na zenye mwanga wa kutosha halafu pia hata waandishi watafaidika na picha wanazopiga, huwa zinatoka safi wakati wa usiku na mahali penye mwanga kama pale uwanjani,” alisema kocha huyo mzungumzaji sana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic