April 24, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema amekubaliana na Zacharia Hanspope na huenda akabaki Simba.

Logarusic amesema amekutana na Hanspope ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na wamezungumza na kukubaliana.
“Nitabaki Simba kwa makubaliano yetu hasa kama yatatekelezwa, nimezungumza na Hanspope, tumekubaliana.
“Lakini nalazimika kurudi nyumbani kwanza, nitaondoka kesho asubuhi kwenda Croatia na baada ya hapo nitasubiri makubaliano yetu,” alisema Logarusic.
Alipoulizwa walichokubaliana na Hanspope ambaye imeelezwa anatarajia kugombea uenyekiti, alisema.
“Tumezungumza mambo mengi, lakini vizuri mkawasiliana naye na kujua tulichokubaliana. Yeye ndiye anaweza kuzungumza,” alisema, kocha wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya.
Mkataba wake ulikuwa ni wa miezi sita tu baada ya kuichukua Simba katika mzunguko wa pili.
Pamoja na kuiwezesha kuitwanga Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Logarusic alishindwa kutamba kwenye Ligi Kuu Bara na kumaliza katika nafasi ya nne.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic