April 17, 2014



Real Madrid ndiyo mabingwa wa Kombe la Mfalme wa Hispania maarufu kama Copa Del Rey na shujaa ni mchezaji ghali zaidi duniani, Gareth Bale.

Kwa ushindi huo, Real Madrid imeshinda kombe lake la 20 la Copa del Rey wakati Barcelona inaendelea kuongoza kwa kushinda mara 26 ikifuatiwa na Atletico Bilbao iliyolibeba mara 23.

Mwaka 2012 kombe hilo lilichukuliwa na Barcelona, mwaka jana wakalibeba Atletico Madrid na sasa limerudi mikononi mwa vijana hao weupe kama yangeyange.

Bale ndiye aliyefunga bao la ushindi katika mechi hiyo iliyopigwa leo, akifunga bao hilo baada ya kukimbia umbali wa mita 40 baada ya kumtoka beki, Marc Bartra wa Barcelona na kufunga bao hilo katika dakika ya 84.
Bao la kwanza la Madrid lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 11 baada ya kuwalaghai mabeki wa Barcelona kama alikuwa anampa mpira Karim Benzema aliyekua kulia kwake lakini akapiga langoni na ukamshinda Pinto.
Bao hilo lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza, Barcelona wakaanza kipindi cha pili kwa kasi kubwa na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 68 kwa kichwa kupitia beki wake, Bartra.
Cristiano Ronaldo ambaye ni majeruhi alionekana kuwa ni mwenye furaha sambamba na Khadeira ambao walikuwa wamenkaa pamoja wakifuatilia mechi hiyo uwanjani hapo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic