April 23, 2014



LIVERPOOL inaelekea ukingoni kwenye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 80 zinazoihifadhi kileleni.

Kama Liverpool itafanikiwa kushinda mechi yake ya Jumapili ijayo dhidi ya Chelsea, maana yake itakuwa imemaliza kumla ng’ombe mzima, mkia itakuwa ni kazi ya mwisho, ishindwe yenyewe.

Lakini hauwezi ukataja ilipofikia Liverpool bila ya kumjumuisha bwa’mdogo Raheem Shaquille Sterling ambaye amekuwa chachu ya mashambulizi ya kikosi hicho.
Kwa sasa, Sterling ni kati ya wachezaji wanaoifanya safu ya ushambuliaji kuwa kali zaidi kuliko nyingine England, kwani katika mechi 35 Liverpool imepachika mabao  96 ambayo ni mengi zaidi kufungwa kwa msimu huu. Man City inafuatia ikiwa na mabao 96.

Sterling  aliyejiunga na Liverpool mwaka 2010 akiwa kinda kabisa ameshaichezea timu hiyo mechi 57 na kufunga mabao 11. Na msimu huu ndiyo ameanza kuonyesha kuwa ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa.
Asili yake ni Jamaica alikozaliwa miaka 19 jijini Kingston, Jamaica. Sterling aliyelelewa na bibi yake kabla ya kuhamia England na mama yake akiwa na umri wa miaka mitano na taratibu alianza kuchukia kisoka.
Sifa zake mbili kubwa ni kasi pamoja na uwezo wa kuuhifadhi mpira na kujua nini cha kufanya tena kwa kasi kubwa.
Uwezo alionao na utofauti na wachezaji wengine ndiyo ulimvutia Kocha Brendan Rodgers kuanza kumpanga hata katika mechi ngumu huku baadhi ya wakongwe wa Liverpool wakipinga kwamba hakuwa ameiva.
Rodgers alipata ushindani mkubwa kwa kuwa wakati alifikia wakati fulani alianza kumuweka nje Daniel Sturridge na kumpanga Sterling ambaye alionekana kama alikuwa hana mchango.
Lakini katika mechi nane za mwisho ambazo Liverpool imeshinda zote na kuwa timu yenye rekodi nzuri ya ushindi mfululizo msimu, Sterling ndiye amekuwa kiongozi wa kuanzisha mashambulizi na ikiwezekana kufunga mabao.
Miaka 19 tu, Sterling ameonyesha ana uwezo mkubwa kwa kuwa katika dakika zake 1,960, tayari amekuwa tegemeo tena akiwa na umri wa miaka 19 tu.
Takwimu zinaonyesha amepiga mashuti 33, kati ya hayo 22 yamelenga lango huku mguu wake wa kulia ukionyesha kuwa ndiyo una uwezo zaidi. Kwani katika mabao yake 9, sita amefunga kwa kulia na matatu kwa kushoto.
Lakini ana kasoro kadhaa kama nguvu hasa anapokutana na mchezaji mwenye nguvu na kasi, lakini ana uwezo wa chini sana katika upigaji vichwa kwa kuwa hana hata bao moja la kichwa.
Kwa maana ya nidhamu ni mmoja wa wachezaji wenye nidhamu ya juu uwanjani, kwani kwa msimu mzima ana kadi moja tu ya njano. Wachezaji wenzake wamekuwa wakimsifia kwamba hata mazoezini ni msikivu sana.
Lakini anashangaza wengi, kwamba nje ya uwanja anaonekana anapenda sana ‘watoto’ lakini ana tabia za watu wa ‘Musoma’ za kuwatandika warembo anaokuwa na uhusiano nao.
Sterling anayelipwa kitita cha pauni 30,000 kwa wiki, amewahi kupandishwa kizimbani mara mbili kutokana na vituko vyake vya kuwatandika wapenzi wake.
Miaka 19, tayari amepanda kizimbani mara mbili kutokana na kuwapiga wapenzi wake wawili tofauti kwa nyakati tofauti.
Mara ya kwanzaalipandishwa kizimbani mwaka juzi, lakini mambo yalipelekwa chinichini kutokana na umri wake kutofikia miaka 18, watu wakamalizana ‘kibingwa’.
Mara ya pili ilikuwa Agosti 8, 2013 alikamatwa kwa kumdhalilisha mpenzi wake mwanamitindo na ilielezwa alimpiga, lakini Septemba 20, mwaka huo, mahakama ikaamua kuwa hakuwa na hatia baada ya kutokuwa na ushahidi.
Lakini bado amekuwa mtu wa mikasa, kwani amewahi kupandishwa pia kizimbani kwa madai ya kukwepa kodi  na ushiriki wake mdogo katika masuala ya jamii.

Usimuona ana umri mdogo au umbo dogo, Sterling ni baba wa mtoto mmoja wa kike aliyezaliwa mwaka 2012 baada ya uhusiano wa muda mfupi tu na msichana ambaye sasa si mpenzi wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic