April 15, 2014


Manchester City ndiyo klabu inayilipa mshahara bomba kuliko nyingine zote duniani.
Klabu hiyo kila mwaka inamwaga pauni milioni 5.3 kwa ajili ya mishahara ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kulipwa.

Wastani wa mshahara kwa wachezaji wake ni pauni 102,653 kwa wiki ambao ni wa juu zaidi.
Timu tano za Ligi Kuu England zimeingia kwenye 20 bora ya timu zinazolipa vizuri duniani.
Liverpool ambao ni wapinzani wakubwa wa City katika kuwania ubingwa wa England, wako katika nafasi ya 20 wakiwa na wastani wa pauni milioni 3.4 kwa mchezaji kwa mwaka.
Manchester United  iko namba nane, wastani wa pauni milioni 4.3 kwa mwaka kwa mchezaji, Chelsea wako nafasi ya 10 kwa wastani wa takribani pauni milioni 4 kwa mchezaji kwa mwaka na Arsenal ni namba 11 kutokana na wastani wa pauni milioni 3.9 kwa mchezaji kwa mwaka.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic