April 17, 2014



Mshambuliaji Emmanuel Okwi hataichezea Yanga tena msimu huu baada ya kocha Hans van Der Pluijm kumtema rasmi.
Kutokana na uamuzi wa kocha huyo, maana yake Okwi ataikosa mechi ya kufunga ligi kuu dhidi ya wapinzani wao Simba, keshokutwa.

Pluijm raia wa Uholanzi, amemuacha OKwi katika kikosi chake kilichoweka kambi kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam baada tu ya kurejea ikitokea Arusha.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, kocha huyo alihimiza Okwi aingie kambini kabla hawajaenda kambini kwenda Arusha, la sivyo hapampa nafasi ya kucheza.
Lakini baadaye Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali akaongeza kuwa kweli Okwi pamoja na Niyonzima hawataivaa Simba, Jumamosi.
“Niyonzima ni mgonjwa kama ilivyo kwa Bahanuzi ambaye anaumwa malaria lakini Okwi hakuingia kambini tokea tunakwenda Arusha, kocha kasema haitakuwa sahihi. Hivyo hatakuwepo.
"Mwingine ambaye hatakuwepo ni Kaseja ambaye pia hakuwepo kambini,” alisema.
Okwi amekuwa akiweka mgomo kwa kuwa anaidai Yanga dola 40,000 ambazo hajamalizia kwenye usajili wake uliogharimu dola 100,000.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic