April 19, 2014


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema wala hana sababu ya kuwa na hofu kutokana na kumkosa Emmanuel Okwi.
Pluijm amesema hafanyi kazi kwa kuangalia majina makubwa na badala yake mchezaji gani anayejituma mazoezini.

Akikosekana Okwi huwezi kusema Yanga haiwezi kucheza, tumeshinda mechi kadhaa bila ya kuwa na Okwi au wachezaji wengine.

Yanga ni timu, haiwezi kuwa inamtegemea mtu mmoja ndiyo maana nimesisitiza sipendi kumzungumzia sana, alisema.

Okwi ameendelea na mgomo wake wa kususia kuichezea Yanga kwa kuwa anadai dola 40,000 zake za usajili.

Awali kulikuwa na mazungumzo kati yake na uongozi wa Yanga, lakini ghafla mambo yakawa kimya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic