July 29, 2014


TEVEZ AKIWA NA SEGUNDO SIKU CHACHE HUKO NYUMA...

Baba wa mshambuliaji wa Juventus, Carlos Tevez aliyekuwa ametekwa amechiwa baada ya watekaji kulipwa kiasi kikubwa cha fedha.

Ingawa imekuwa ni siri kiasi gani wamelipwa, lakini magazeti ya Argentina na vyombo vingine vya habari vimeeleza, familia ya Tevez imelazimika kutoa mamilioni ya fedha kumuokoa Segundo Tevez.
Baba huyo alitekwa baada ya gari alilokuwa akisafiria kuzuiwa na watekaji hao katika eneo la Morón, Magharibi mwa jiji la Buenos Aires.
Mwanasheria wa familia ya Tevez, Gustavo Galass, amesema Segundo Tévez alitekwa na wahusika wakapiga simu kwenye familia hiyo na kudai fedha huku wakitoa saa nane tu kabla ya kuchukua uhai wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic