Klabu ya Al
Shaolla ya Saudi Arabia imeamua kusitisha mkataba wake na makocha Hans van der
Pluijm raia wa Uholanzi na Charles Boniface Mkwasa, Mtanzania.
Habari za
uhakika kutoka Saudi Arabia zimeeleza kumetokea hali ya kutoelewana kati ya
makocha hao na uongozi.
SALEHJEMBE,
imefanya juhudi za kuwasaka wawili hao hadi ilipompata Mkwasa ambaye ametoa
ufafanuzi.
Mkwasa
amesema tatizo lililosababisha wao
kuingia kwenye mzozo ni suala la usajili.
“Kweli hapa
hali imebadilika ghafla baada ya kocha na uongozi kushindwa kuelewana kutokana
na usajili wa wachezaji wapya kwa msimu ujao.
Viongozi waliwaleta wachezaji kwa
majaribio ambao kwa muono wa kawaida hawakuwa na uwezo mzuri.
“Kwa ujumla
tuliwakataa na pia walikuwa wanataka wachezaji kutoka madaraja ya chini pia
walikataliwa, wao hawakupendezewa nalo hivyo wakaamua kusitisha mikataba yetu
kwa sababu kubwa wanasema hawana fedha,” alisema Mkwasa na kuendelea kufafanua.
“Msimu
uliopita timu hii ilishika nafasi ya 12 ambayo ni timu ya mwisho kubaki daraja
hivyo coach Hans alitaka wasajili wachezaji wenye uwezo ili waweze kufanya
uzuri, kama haitoshi wachezaji wachache wazuri wa Shoulla wa msimu uliopita nao
walihama so timu ilikuwa inahitaji wachezaji wengi na wa hali ya juu.
“Habari ndiyo
hiyo, likiharika lawama kwa kocha usajili wanataka wa chee.
Taratibu za safari
ya kurudi makwetu zinafanyika.”
Pluijm ndiye
alianza kujiunga na Shoulla kabla ya kumpendeleza Mkwasa ambaye alifanya naye
kazi Yanga kwa ufasaha.
0 COMMENTS:
Post a Comment