July 31, 2014


Daniel Craig maarufu kama James Bond ameonyesha wazi mapenzi yake kwa Liverpool.
Muigizaji huyo maarufu wa filamu za James Bond alikuwa katika mechi ya kujipima nguvu kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City jijini New York, Marekani.
Wakati mechi ikiendelea, Craig alikuwa akionyesha kukasirishwa kama mwamuzi ‘ameiuma’ Liverpool.

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya mabao 2-2, Liverpool wakisawazisha dakika ya 85 kupitia Raheem Sterling.
Baada ya hapo, James Bond alikwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya Liverpool, akapiga stori na wachezaji, halafu akapicha picha na nahodha Steven Gerrard.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic