July 25, 2014



Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, juzi Jumatano aligeuka kuwa kivutio kwa mashabiki waliojitokeza kuangalia mazoezi ya timu yake, Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar baada ya kuanza kuigiza kazi ya utangazaji mpira.


Katika mazoezi hayo, wachezaji wa Yanga waligawanywa katika timu mbili kisha Maximo akasimama pembeni ya uwanja, akifuatilia kilichokuwa kikiendelea, ambapo baada ya muda, alianza kutaja majina ya wachezaji wake kila ambaye alikuwa akigusa mpira.

Kuona hivyo, mashabiki waliokuwa karibu yake wakaanza kuangua vicheko kutokana na Maximo kutamka majina kama mtangazaji wa mchezo wa soka.

Mbrazili huyo hakujali vicheko hivyo, badala yake aliendelea na majukumu yake kama kawaida na wakati mwingine kujikuta akitamka maneno kadhaa katika lugha tatu tofauti, Kiswahili, Kiingereza na Kireno.

“Jamaa anaburudisha sana jinsi anavyoyatamka majina ya wachezaji wake, huwezi kuamini kama amekaa na timu kwa muda mfupi tu,” alisikika mmoja wa mashabiki hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic