KIIZA (KUSHOTO) |
Kocha Marcio Maximo sasa ndiye atakayeamua kuhusiana na Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza, lakini baada ya kufanya nao kazi angalau kwa wiki moja.
Huenda wakaungana na Yanga jijini Dar es Salaam au mjini Pemba.
OKWI |
Okwi na Kiiza wanalazimika kugombea nafasi moja ya wachezaji wa kimataifa iliyobaki.
Uongozi wa wote wanatarajiwa
kutua nchini ndani ya siku chache zijazo kuanza kazi na kocha mpya, Marcio
Maximo, imefahamika.
Uongozi wa Yanga umeamua kulikabidhi suala hilo kwa Maximo, ambaye mwisho ataamua kwamba abaki na Okwi au Kiiza.
“Kwa kuwa ameachiwa Maximo, yeye kama kocha ametaka wote waje
kazini na mwisho ataamua yupi kati yao atakuwa anamhitaji kutokana na kikosi
chake kinahitaji nini.
“Hivyo wote watakuja na kuungana na wenzao mara tu watakapomaliza
majukumu ya kikosi cha timu yao ya taifa,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Yanga imekuwa haijui imuache nani kati ya Okwi au Kiiza ili
kumuachia nafasi Jaja, mshambuliaji mpya kutoka Brazil. Kwa mujibu wa Sheria za
TFF, wachezaji wa kigeni wanatakiwa kuwa ni watano tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment