July 24, 2014


SAID MECK SADIQ, MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM (KULIA) AKIWA NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO, FAROUK BAGHOZA (ANAYEMFUATIA), WENGINE NI WAJUMBE WA KAMATI HIYO, SAAD KAWEMBA NA HAGILA.

Kamati inayoshughulikia ujio wa klabu kongwe duniani ya Real Madrid, leo imetua kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq na kupata baraka.
Sadick ametoa Baraka zake kwa kamati hiyo kuhusiana na ujio wa wa Real Madrid ya wakongwe.
Mkuu huyo wa mkoa, amewatakia maandalizi mema watu hao wa kamati.

“Kweli tumepata Baraka za mkuu wa mkoa ambaye ndiye baba wa mkoa wetu. Ametupa Baraka tuendelee na maandalizi ambalo ni jambo jema.

“Tumefurahi na nguvu ya kuendelea kufanya jambo hilo imeongezeka, nyie mnasema morali. Hivyo tunaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Ssebo ambaye ni mratibu wa ziara hiyo.

Wakongwe hao wa Real Madrid wanatarajia kutua nchini na kukipiga Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ssebo alisema maandalizi yanaendelea vizuri na wanatarajia kupata sapoti ya Watanzania pamoja na makampuni kuhusiana na ugeni huo mkubwa wa kimichezo nchini.

Wachezaji nyota wa zamani wa Real Madrid wanaoounda kikosi hicho wakiwemo Luis Figo na wenzake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic