July 19, 2014

KWIZERA (KATIKATI) BAADA YA KUTUA UWANJA WA TAIFA, KUSHOTO NI MEDDY NA KULIA NI IDDI KAJUNA.


Kiungo nyota wa timu ya taifa ya Burundi, Pierre Kwizera ametua nchini tayari kuanza kazi na Simba.

Kwizera ambaye anakipiga timu ya Afad Abidjan inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ivory Coast, tayari yuko Dar.
Alitua nchini na kupokelewa na kiongozi wa Simba aitwaye Meddy na Iddi Kajuna. 
Mrundi huyo rasmi ataanza rasmi mazoezi Jumatatu.
Simba iliamua kumchukua kiungo huyo badala ya Jerry Santo raia wa Kenya ambaye ilifanya naye mazungumzo kwa asilimia 90.
Pamoja na sifa ya pasi za uhakika na ukabaji, Kwizera anasifika kwa kupiga mashuti makali nje ya 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic