July 30, 2014

MWAIKIMBA AKIWA NA KIPRE TCHETCHE


Straika mkongwe wa Azam, Gaudence Mwaikimba, amemwambia straika mpya wa timu hiyo, Didier Kavumbagu kuwa anakwenda kujifunza kutoka kwake.


Kavumbagu alijiunga na mabingwa hao katika dirisha hili la usajili akitokea Yanga sambamba na Frank Domayo, ambapo ameifanya safu ya ushambuliaji kuwa na hofu kubwa ya namba kwa sasa.

Mwaikimba alikiri kuwa Kavumbagu ameongeza ushindani wa namba, lakini kwake si lolote kwani ni kama amekuja kujifunza mengi kutoka kwa mkongwe huyo kuliko mchezaji yeyote.

Mwaikimba, ambaye amedumu kwenye ligi kuu kwa zaidi ya miaka kumi, amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Azam, hususan katika mechi za mikoani ambapo mastraika wengi wa Simba, Yanga na Azam pamoja na maprofesheno wengine, wamekuwa wakichemka.

“Kwanza Kavumbagu ana bahati kubwa kuja kipindi hiki, maana ana nafasi ya kujifunza mengi kutoka kwangu. Mimi ni mkongwe na kuna vitu vingi ambavyo atajifunza kutoka kwangu, ingawa na mimi vipo ambavyo nitajifunza kutoka kwake.
“Kweli ameleta changamoto katika suala la namba, lakini pia ni faida kwa wote kwani ni kipindi cha kila mchezaji kujituma mara mbili ili kupata namba kikosi cha kwanza,” alisema Mwaikimba.
Ujio wa Kavumbagu, pamoja na Mhaiti, Leonel Saint Preux, umeifanya safu ya ushambuliaji ya Azam kuwa na watu saba, wakiungana na Kipre Tchetche, John Bocco pamoja na makinda Joseph Kimwaga na Kelvin Friday.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic