July 29, 2014

MWOMBEKI (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA MABEKI WA PRISONS.

Mshambuliaji mpya wa JKT Ruvu, Betram Mwombeki amesema yuko katika kiwango kizuri na anatamani kukutana na Simba ya Zdravko Logarusic na kuonyesha uwezo.


Mwombeki aliondoka Simba baada ya Loga kusisitiza kutomtaka katika kikosi chake.
Mshambuliaji huyo alionekana msaada mkubwa kabla ya kutua kwa Loga ambaye hakuelewana naye.
Mwombeki amesema ana mapenzi makubwa na Simba na anatamani kurudi na kufanya kazi katika kikosi hicho.
“Uwezo ninao, ninachotaka ni kufanya vema na siku ikifika, nitarudi tena.
“Nimefanya mazoezi sana, ninaendelea kujifua lakini lengo ni kufanya vizuri,” alisema straika huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa akiwa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic