July 28, 2014



UJIO wa Real Madrid nchini umeonyesha kuwachanganya watu wengi na hasa wale wa mikoani.
Baadhi ya wadau wa soka kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Tanga na Morogoro wametuma barua pepe katika SALEHJEMBE wakitaka ufafanuzi.
Real Madrid inatarajiwa kutua nchini Agosti 22 kabla ya kukipiga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Agosti 23.

Wadau hao wamekuwa wakihoji kama kweli wachezaji kama Luis Figo, Michael Owen na wengine wanaochezea kikosi cha Madrid ya wakongwe wanaweza kweli kuja nchini.

“Ningependa kupata ufafanuzi, kweli inawezekana hao jamaa wakaja hapa nchini, au ni maneno tu halafu mwisho tutaambiwa imeshindikana,” alihoji John Shilinde wa Shinyanga.

“Mimi nataka kusafiri kuja kuwaona hao jamaa, unajua kwa umri wangu mimi ningefurahi kuwaona watu kama Owen, Figo, Zidane na wengine wa ile Madrid ya wakati ule. Sasa uhakika, kweli wanakuja,” alihoji Mohammed Salim wa Tanga.

SALEHJEMBE ilimsaka mratibu wa ziara hiyo kupitia kampuni ya TSN Supermarket, Ssebo ambaye alielezea jambo hilo.

“Waambie hakuna suala la kubahatisha na maandalizi yanakwenda vizuri ndugu yangu.

“Unakumbuka mwanzo tulizungumzia suala la ushirikiano tunaoupata kwa serikali na tulikwenda kwa mkuu wa mkoa.

“Tunamshukuru sana kiongozi wa juu wa mkoa wa dare s Salaam. Lakini mambo yanakwenda vizuri na tunafanya kila linalowezekana ili mambo yaende sawa,” alifafanua Ssebo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic