July 25, 2014



Kipa wa Coastal Union, ShabanI Kado amejikuta akiacha gumzo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook baada ya kutupia picha inayomuonyesha akitumia bunduki.


Kado alitupia picha hiyo kwenye kurasa zake zote mbili za mitandao hiyo, ambapo picha moja ilionyesha akilenga ilipo kamera, ya pili alikuwa ameishika bastola hiyo kulenga kichwa chake na ya tatu ni picha ya bastola ikiwa juu ya meza.

Alipopigiwa simu kuhusiana na suala hilo, Kado alicheka kisha akajibu: “Siyo yenyewe hiyo mwanangu, hilo pambo tu ila ukiitazama ni kama ya ukweli, ipotezee kama vipi.”

 Mara nyingi imekuwa ikionywa kuonyesha silaha hadharani, kitu ambacho kinaweza kusababisha wengi kuamini nyota huyo anaimiliki kweli na kufanya maisha yake kuwa hatarini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic