Msafara wa watu 27
wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu)
saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga
kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho
(Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na baadaye jioni kuunganisha safari
ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya
marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa
Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
Msafara huo wa
Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni
maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka
Uholanzi.
Wakati kiungo
Mwinyi Kazimoto ametua leo (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake,
washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho
(Julai 30 mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati huo huo,
Serengeti Boys imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg,
Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 17 dhidi Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya
marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za
Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka
suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Dar es Salaam. Serengeti Boys inahitaji ushindi kwenye mechi hiyo
au aina yoyote ya sare ya mabao ili ifuzu kwa raundi ya tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment