July 30, 2014



Kikosi cha Taifa Stars, kinatarajiwa kuondoka nchini leo Jumatano, kuelekea Msumbiji lakini kitaweka kambi ya muda mfupi Afrika Kusini ambapo kitaungana na washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.


Stars inakwenda Msumbiji kwenye mchezo wa marudiano wa kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco mwakani.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa siku chache zilizopita, Stars ilijikuta ikimaliza vibaya baada ya kuambulia sare ya mabao 2-2 na sasa itatakiwa kuhakikisha inaibuka na ushindi au sare ya zaidi ya mabao hayo.

Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema timu hiyo inatarajia kuondoka nchi leo Jumatano kwa ajili ya kuelekea nchini Msumbiji katika mchezo huo wa Jumapili.

“Timu inatarajiwa kuondoka nchini leo kuelekea Maputo Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa marudiano ambao utachezwa siku ya Jumapili, lakini itapumzika kidogo Afrika Kusini ambapo itaungana na Samatta na  Ulimwengu ambao wanacheza TP Mazembe ya Congo.

 “Kwa upande wa kikosi, wachezaji wote wapo vizuri na jana wamefanya mazoezi kama kawaida, naamini kuwa tutaibuka na ushindi kwenye mchezo huo,” alisema Mwesigwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic