Ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Azam FC hasa kwenye safu ya
ushambuliaji unazidi kuwa mkali ambapo sasa kila mmoja amejinadi kufanya vizuri
ili kumshawishi kocha ampange katika kikosi cha kwanza.
Kipre Tchetche, raia wa Ivory Coast, amefunguka kuwa, hana hofu juu
ya nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza lakini akaongeza kuwa, anafurahia
ushindani kwa kuwa ni kwa faida ya timu yake.
Safu ya ushambuliaji ya Azam FC sasa inaundwa na Kipre, Didier
Kavumbagu raia wa Burundi, Leonel Saint Preux wa Haiti na Watanzania John
Bocco, Gaudence Mwaikimba na Kelvin Friday.
“Kuwepo kwa mastraika wengi katika kikosi chetu ni moja ya mafanikio
na kuongeza ushindani, nitaendelea kujituma lakini naamini uwezo wangu upo juu.
“Lakini kikubwa ni kuwa
tunajipanga vema kuhakikisha tunafanya vizuri, ujio wa wachezaji wapya ni mzuri
na ujue kuwa hakuna mchezaji ambaye namhofia,” alijinadi Tchetche ambaye
alishika nafasi ya pili kwa ufungaji katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment