August 22, 2014



Kocha na beki wa zamani wa Simba, Amri Said ‘Jaap Stam’ ambaye alikuwa msaidizi wa Patrick Phiri wakati akiinoa Simba mwaka 2010, amemuomba Phiri kuhakikisha anamrejesha Haruna Moshi ‘Boban’ baada ya kuona upungufu kikosini hapo.


Boban kwa sasa hana timu tangu aachane na Coastal Union, kwa sababu zake binafsi, hata hivyo msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.

Stam ambaye amewahi kuifundisha Ndanda FC, amesema Phiri ni kocha mwenye uwezo wa kuishi na watu watukutu, ambapo alimudu kuishi naye mwaka 2010.

“Phiri anamjua Boban, wengi wamekuwa wakishindwa kuishi naye kutokana na utukutu wake, lakini kumbuka enzi zetu nikiwa na Phiri tuliweza kukaa naye na kufanya kile Wana-Simba walitamani.

“Pamoja na kwamba nimeondoka Simba, lakini ukweli ni kwamba Phiri anahitaji kuwa na mtu kama Boban, maana anamfahamu vema utukutu na kiwango chake,” alisema beki huyo wa zamani wa Simba. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic