August 26, 2014



Ungekuwa wewe ungevunga lakini si Cristian Karembeu wa Real Madrid. Mara tu baada ya kumfikia Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, fasta akaomba apewe ‘shavu’.

Karembeu ambaye alikuwa nchini na kikosi cha wakiongwe cha Real Madrid, alimuomba Rais Kikwete wapige picha pamoja kutumia ‘tab’ yake.
Rais kwa kuwa ni mtu wa watu, wala hgaikuchukua hata sekunde, akasogea na Karembeu akafyatua ‘ta, ta, ta’.
Picha hiyo kwa ajili ya kumbukumbu, Karembeu ambaye kikosi chake siku hiyo kiliichapa Tanzania Eleven 3-1, anaweza kujidai nazo Facebook, Twitter au Instagram.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic