Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza
mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha
kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico
Madrid.
Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya
pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao
2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou.
Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic
ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo
katika dakika ya 2 tu.
Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti
kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza
kupindua matokeo.
Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment