August 27, 2014


 Kweli Mario Balotelli haishi vituko, tayari ameanza mazoezi na Liverpool, lakini vituko kama kawa.
Balotelli ametumia zaidi ya dakika moja eti akisumbuka kuvaa bib ya mazoezi, wakati huo wenzake wakiendelea na mazoezi.

Lakini kama hiyo haitoshi, ingawa ndiyo siku ya kwanza akiwa na wenzake, tayari ameanza utani kwa kuangushana na Kolo Toure.

Hofu ni moja, Balotelli haeleweki, mara utani, mara ageuke ‘shoziniga’. Mashalah yake ni shiiiida.
Wakati Liverpool ikiendelea na mazoezi, mashabiki wanaoishi nyumba jirani walishindwa kujizua baada ya kupanda ukuta ili washuhudie kama ni kweli Balotelli yuko mazoezini.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic