August 30, 2014

BANDA (KUSHOTO) AKIWA MAZOEINI SIMBA PAMOJA NA BEKI JOSEPH OWINO.


Timu ya Coastal Union ya Tanga, imesema itafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha mchezaji wao, Abdi Banda anaichezea timu hiyo msimu ujao na siyo Simba.


Tayari beki huyo ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea Simba na inaeleweka wazi kuwa Simba watawasilisha jina lake kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa, baada ya kudai kuwa alishamaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Tanga.

Awali uongozi wa Coastal, ulipeleka malalamiko yake kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulalamikia juu ya mchezaji wao kusajiliwa na Simba lakini maamuzi bado hayajatolewa.

Ofisa Habari wa Coastal, Oscar Asenga, amesema kuwa wameorodhesha jina la beki huyo kwenye majina ya usajili wa wachezaji wao watakaowatumia msimu ujao.

“Tutafanya kila tutakaloweza ili kuhakikisha anakuwa mchezaji wetu, ndiyo maana katika orodha ya wachezaji tuliyoiwasilisha TFF, jina la beki wetu Banda lipo na Simba watambue hatutakubali mchezaji wetu aichezee timu yao,” alisema Asenga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic