August 20, 2014



Kocha wa Brazil, Dunga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya ya mechi za kirafiki dhidi ya Colombia, mechi itakayopigwa Septemba 5 jijini Miami, na dhidi ya Ecuador Septemba 9 jijini New Jersey, Marekani.


Kati ya wachezaji aliowaita ni Miranda wa Atlético de Madrid na Filipe Luís.
Lakini Dunga akaamua kuwaacha mabeki Dani Alves wa Barcelona na Marcelo wa Real Madrid.
Nahodha Thiago Silva anayekipiga PSG pia ni mgonjwa, hivyo pia amemuacha katika kikosi chake.
Wachezaji waliocheza Kombe la Dunia 2014 ambao Dunga amewaita ni Jefferson, David Luiz, Maicon, Luiz Gustavo, Fernandinho, Ramires, Oscar, Hulk, Willian and Neymar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic