August 22, 2014

FAROUK (KATIKATI) AKIZUNGUMZA HUKU FIGO (KULIA) NA SANZ WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI LEO KATIKA HOTELI YA SOUTHERNSUN JIJINI DAR.


Mshambuliaji nyota wa timu ya wakongwe ya Real Madrid, Luis Figo amesema anaiheshimu timu ya wakongwe ya Tanzania Eleven.
Lakini akasisitiza kuwa mechi ya kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar itakuwa ngumu.
FIGO AKIZUNGUMZA HUKU KAREMBEU, SANZ NA JULIO WAKIMSIKILIZA. KULIA NI MWENYEJI WAO, BOSI MKUBWA KABISA WA TSN, FAROUK BAGHOZA. ALIYESIMAMA NI DENIS SEBBO, MRATIBU WA ZIARA HIYO
“Lazima niseme ninaheshimu kikosi cha wakongwe wa Tanzania, tunaamini itakuwa mechi nzuri nay a ushindani sana,” alisema Figo.

Lakini kiungo Cristine Karembeu amesema atatoa pasi nyingi kwa Figo ili atumie kipaji chake na kufunga.

“Unajua Figo ana kipaji, tutakitumia kwa kumpa pasi nyingi zaidi ili afunge mabao.

“Mechi haitakuwa lahisi kama alivyosema Figo, ila tunawaomba wasipanie sana ili tutoe burudani kwa Watanzania,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TSN, Farouk Baghoza amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo.
Baghoza amesema Watanzania watakapojitokeza kwa wingi, itakuwa ni furaha na tiketi zimeanza kuuzwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic