August 27, 2014



Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog amewaita wachezaji wake kuanza mazoezi kesho ili kumalizia maandalizi ya msimu mpya.

Meneja Azam FC, Jemedari Said amesema kikosi chake kitaanza mazoezi kesho.
Wachezaji ambao hawakuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa wataanza mazoezi.
“Baada ya hapo, wale ambao walikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, pia wataungana na wenzao,” alisema Jemedari.
Omog alitoa mapumziko kwa wachezaji wake mara baada ya michuano ya Kagame nchini Rwanda.
Azam FC ilitolewa kwenye michuano hiyo katika hatua ya robo fainali dhidi ya El Merreikh ya Sudan ambayo ndiyo imeibuka na kuwa bingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic