August 31, 2014



Cristiano Ronaldo ameamua kufunguka kuhusiana na uhusiano wake na Kocha Jose Mourinho na kusema hakuwahi kuwa rafiki yake hata chembe.

Licha ya Mourinho kuwahi kuwa rafiki yake na raia mwenzake wa Ureno, Ronaldo amesema hajawahi kuwa na urafiki naye, badala yake akasisitiza katika makocha, rafiki yake ni mmoja tu, Alex Ferguson aliyekuwa naye Manchester United.
Aidha, Ronaldo amemlaumu Mourinho kwamba wakati akiwa kocha wa Madrid alisababisha mambo mengi kama ugomvi kati ya wachezaji na hata mashabiki.
Mourinho hakuelewana na Iker Casillas, Angel Di Maria, Sergio Ramos na hata Mreno mwenzake, Pepe.
Ronaldo amesema Mourinho alifanya hali ya hewa kutotulia ndani ya kikosi chao huku akisisitiza hayuko kwenye soka kutafuta marafiki, badala yake anataka kushinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic