August 1, 2014


UJUMBE WA KAMATI YA MAANDALIZI YA REAL MADRID UKIWA NA WAZIRI MUKANGARA.

Baada ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamati ya maandalizi ya ujio wa kikosi cha wakongwe wa Real Madrid, imetua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Fenella Ephraim Mukangara.
Ujumbe huo umetua ofisini kwa Waziri Mukangara na kufanya mazungumzo naye, pia kumuelezea kuhusiana na ujio wa Madrid, Agosti 23.
Ujumbe huo ulioongozwa na bosi mkubwa kabisa wa TSN, Farough Baghoza ulipata nafasi ya kuzungumza na Waziri Mukangara ambaye ametoa baraka zake.
Kama ilivyoeleza awali kwamba serikali inashirikiana na kati hiyo bega kwa bega ndivyo imetokea kwa Waziri Mukangara ambaye ameahidi kushirikiana nao katika ugeni huo mzito.

Tayari ujio wa Madrid umekuwa gumzo kubwa huku mashabiki wengi wakiwa na hamu ya kuwaona nyota hao wakongwe wa Madrid ambao watakuwa wanatua Afrika kwa mara ya kwanza na Tanzania ikiwa ni nchi ya kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic