August 21, 2014



Hamisi Chokwa, Pemba
Kocha Marcio Maximo ameanza mechi yake ya kwanza akiwa na Yanga kwa ushindi wa bao 1-0.
Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba uliochezwa kwenye Uwanja wa Gombani mjini hapa.
Bao la pekee Yanga katika mechi hiyo lilifungwa katika dakika ya 6 na mshambuliaji wake Mbrazil, Jaja.
Jaja alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kuruka juu na kuuwahi mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Maximo alikuwa akibadili wachezaji mfululizo akionyesha alikuwa amepania kuona jambo fulani.
Hiyo ndiyo mechi ya kwanza kwa Yanga kucheza ikiwa chini ya Maximo ambaye awali alikataa mechi za kirafiki akitaka kwanza kujenga kikosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic