September 18, 2014


Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi Tambwe amesema miguu yake na kichwa, kitatoa majibu ya kila swali msimu ujao.


Tambwe raia wa Burundi amesema bado ana uwezo wa kufunga mabao na ana nafasi ya kuwaonyesha wanaombeza.

"Mambo mengine tunamwachia Mungu, lakini mimi ninajiamini. Ndiyo maana nasema kichwa na miguu itaongea.

"Unajua mpira ni kitu kigumu au kinaweza kuwa lahisi kutokana na mnavyoshirikiana. Kwa hapa Simba tunaelewana vizuri sana kiuchezaji.
"Bado nina imani tukicheza kwa mechi mbili tatu zaidi tutakuwa tishio," aisema Tambwe.

Mrundi huyo aliibuka mfungaji bora wa msimu uliopita baada ya kufunga mabao 20.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic