September 17, 2014

PONDAMALI AKIFAFANUA KWA MHARIRI WA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI KUHUSIANA NA SUALA LA USHIRIKINA.

Unaweza kusema vitu havitokei au ni hadithi tu, lakini wakati mwingine unakutana navyo kama alivyosema kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, kuwa uchawi unatumika kwenye soka naye anauamini.

Pondamali maarufu kama Mensah amesema uchawi upon a unatumika sana kwenye Ligi Kuu Bara huku akisisitiza: “Nimesema, andika.”
Pondamali aliiambia SALEHJEMBE, mbele ya mhariri wa gazeti maarufu la michezo la Championi Jumatano.
“Nyie mnapenda sana kuiga uzungu Saleh, uchawi upon a unatumika kwa sana tu.
“Unakumbuka mimi nilikuwa ninadaka mpira halafu namrudishia mchezaji. Si namponda nao, namrudishia anapiga tena nanyaka.
“Si kitu lahisi, najua kazi ni ngumu sana lakini mtaniamini tu. Uchawi ni utamaduni wa Mwafrika,” alisema.
Alipoulizwa kama naye pamoja na kuamini ni mtu anayefanya mambo ya kishirikina. Pamoja na kuonyesha ni amekuwa mkali ghafla, alihoji.

“Mimi ni Mzungu au Mwafrika, chambua hilo jibu halafu utapata jibu sahihi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic