September 23, 2014


KIONGERA AKIGONGANA NA KADO...
Picha inaonyesha kipa Shabani Kado akimgonga mshambuliaji Paul Kiongera wa Simba wakati wakiwania mpira,

Kiongera raia wa Kenya aliumia na kutolewa nje, Kado akatibiwa na kumalizia dakika moja iliyobaki.
Sasa Kiongera anaikosa mechi ya Oktoba 12 ya watani wao Yanga ambayo inasubiriwa kwa hamu.
ANAANGUKA BAADA YA KUGONGANA NA KADO AMBAYE ANALIA MAUMIVU PIA...

Vipimo vilivyotolewa leo kwenye hospitali ya rufaa ya Muhimbili vimeeleza Kiongera ameumia sana goti lake na tayari imepitishwa apumzike wiki sita.
Hali hiyo imejulikana baada ya daktari wa Simba kusafiri na Kiongera hadi Dar es Salaam wakitoka kambini Zanzibar na kufanyiwa vipimo.
Majeruhi wengine ni Haruna Chanongo ambaye amebakiza siku mbili kabla ya kurudi uwajani na kuanza mazoezi mepesi na Issa Rashid maarufu kama Baba Ubaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic