September 1, 2014



Katika jitihada za kumfanya awe tishio zaidi msimu ujao, benchi la ufundi la Yanga limeamua kumuongezea programu ya mazoezi straika Mbrazil, Genilson Santos ‘Jaja’.


Kuonyesha kwamba Yanga haitaki mchezo, Jaja amekuwa akiendelea kufanyishwa mazoezi hata pale wenzake wanapopumzika.
Yanga, juzi Jumamosi asubuhi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola Mabibo jijini Dar, ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dar iliyomalizika kwa bao 1-1.

Straika huyo aliendelea kukimbia kwa kuzunguka uwanja kama alivyotakiwa na kocha wake, hali iliyowafanya mashabiki waamini kuwa ni muendelezo wa mazoezi ya kumpa wepesi mchezaji huyo kabla ya ligi kuanza Septemba 20, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic