September 19, 2014


Msemaji mwenye mbwembwe wa Mtibwa Sugar, Thobia Kifaru amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya kesho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.



Mechi hiyo inapigwa kwenye Uwanjwa wa Jamhuri mjini Morogoro na amesisitiza kuwa mshambuliaji Jaja wa Yanga, ataonekana kituko.
"Waje kwa wingi wamuone huyo Jaja, waliwafunga Azam FC tatu kwa kuwa hawakuwa vizuri.
"Azam FC walikuwa kama wagonjwa vile, hawakucheza vizuri kwenye kiungo wala ushambuliaji. Sasa wanadhani ndiyo Mtibwa.
"Tutawafunga na Jaja wao, ndiyo maana nataka mashabiki waje kwa wingi sana," alisema Kifaru.
Tayari Yanga imewasili mjini Morogoro kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic