September 30, 2014


Wachezaji wa Bayern Munich, walilazimika kukimbia mbio wakitolewa kwenye hoteli mjini Moscow baada ya kuwa na taarifa ya moto.

Wachezaji hao wakiwa na kocha wao Pep Guardiola walilazimika kutimua mbio hadi nje ya hoteli baada ya kuwa na taarifa kwamba kuna moto kwenye moja ya sehemu ya hoteli hiyo.

Kikosi hicho kipo mjini humo kuivaa CSKA Moscow katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji hao walikutana na wakati mgumu baada ya kutolewa nje ya hoteli kutokana na baridi kali mjini humo.

Hali hiyo iliwalazimu baadhi yao kuchukua mataulo ya hoteli na kujifunika ili kupambana na hali hiyo ya baridi kali.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic