September 28, 2014

MPIRA UMEKWISHAAAAA...
Dk 90+3..Prisons wanapata kona

Dk 89, Juma Abdul analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madambi Chudu.
Dk 87, Prisons wanapata kona lakini inakuwa haina madhara.

Dk 82, Ngassa akiwa peke yake na kipa anashindwa kufunga.


Dk 79, Fred Chudu anashindwa kufunga huku lango la Yanga likiwa wazi
Dk 77, anatoka Yondani anaingia Rajab Zahir

Dk 72, Jaja anapiga shuti kali lakini kipa anaokoa kwa ustadi mkubwa.


Dk 73, Msuva naye anapiga shuti kali lakini anashindwa kulenga.
GOOOOOO Dk 69, Msuva anaifungia Yanga bao baada ya kuunganishwa kwa kichwa krosi safi ya Ngassa.


GOOOOOOO Dk 67, Ibrahim Hassan anaifungia Prisons bao kwa kichwa baada ya kumkimbia Yondani na kufunga kilahisi akiwa peke yake.


Dk 65, Julius Nkwanga anawatoka mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali lakini linapita juu kidogo ya lango la Yanga.


Dk 61, Msuva anapiga shuti kali linatoka sentimeta chache.

Dk 59, Prisons wanafanya shambulizi zuri lakini umaliziaji unakuwa shidaaaa.Dk 57, Yanga wanamtoa Coutinho anaingia Simon Msuva.

Dk 55, Yanga wanamtoa Dilunga anaingia Hamis Thabit

Dk 49, Hassan Dilunga anapiga shuti kali lakini linatoka nje kidogo.

Dk 47, Niyonzima anaingia ndani ya 12, lakini anashindwa kufungwa.
MAPUMZIKO:
Dk 43, Jaja anapiga kichwa safi kilichokuwa kinaelekea langoni, lakini kipa wa Prisons anaokoa.

Dk 38, Jacob Mwalobo anapigwa kadi ya pili ya njano, inazaa nyekundu, anakwenda nje.

GOOOOOOO Dk 34, kupitia mpira wa faulo, Coutinho anafunga bao safi la faulo baada ya Niyonzima kumpisha, naye akaachia mkwaju mkali wa takribani mita 27.

Dk 33, Yanga inaongoza kumiliki mpira kwa 55% na Prisons 45%.

Dk 28, Jaja anaingiza mpira ndani kumtafuta Ngassa lakini kipa anaudaka kwa ustadi mkubwa
Dk 22, Ngassa anawatoka mabeki wa Prisons lakini wanamuwahi na kuutoa mpira, unakua kona isiyo na matunda.

Dk 17, Meshack Selemani anapiga shuti kali linatoka sentimeta chache, ni baada ya Cannavaro kupoteza pasi.


Dk 13, Coutinho anapokea pasi nzuri ya Ngassa lakini shuti lake linapaa juu

Dk 6, Coutinho anawatoka mabeki wa Prisons anapiga pasi safi lakini mabeki Prisons wanaokoa, inakuwa kona isiyo na madhara.


Dk 4 Ngassa anapiga krosi, Jaja anaruka juu lakini anashindwa kuufikia mpira.

Kikosi Yanga:
Dida, Juma Abdul, Edward Charles, Cannavaro, Yondani, Twite, Dilunga, Niyonzima, Jaja, Coutinho na Ngassa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic