September 19, 2014


Pamoja na kuendelea kucheza soka nchini Sweden mshambuliaji Athuman Machuppa ameamua kujiongezea kipato zaidi kwa kufanya kazi za kawaida.
Kwa sasa Machuppa anakipiga katika kikosi kinachoshiriki daraja la pili nchini Sweden cha Armeinska Syrianska.

Mtanzania, Machuppa ambaye aliwahi kung’ara akiwa Simba na timu ya soka ya taifa, Taifa Stars sasa anafanya kazi kwenye Mhahawa mkubwa nchini humo na duniani kote wa MacDonald.
“Kweli nacheza soka na pia nafanya kazi kaka, si unajua maisha ni kujituma,” alisema Machuppa kutoka Stockholm.
Machuppa amekuwa akiishi nchini humo kwa zaidi ya miaka sita akikipiga katika timu mbalimbali.

Wakati akiwa kinda, Machuppa alifahamika kwa kasi, ujuzi na mashuti ya kushitukiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic