September 19, 2014


Simba na Mbeya City zipo hatarini kupanda kizimbani kujibu shitaka la kukiuka kanuni na sheria za Fifa, kwa kitendo cha kutopima afya za wachezaji kabla ya kuanza kuzitumikia kwa msimu ujao.


Kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) zinaeleza kuwa, kila mchezaji ni lazima afanyiwe vipimo vya afya kabla ya kuanza kucheza, agizo ambalo linaonekana kutokuwa na mashiko nchini Tanzania.

Katibu wa Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo Tanzania (Tasma), Nassor Matuzya, ambacho ndicho kinahusika na upimaji wa afya za wachezaji nchini, amesema mpaka jana Alhamisi ni timu tano tu ndizo zilikuwa zimetekeleza kanuni hiyo ambazo ni Yanga, Azam, Coastal Union, Mgambo na Ndanda huku Panone FC ikiwa ni timu pekee kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Matuzya, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Tiba ya TFF, amekwenda mbali na kusema Simba walipewa taarifa mara mbili lakini hawajatekeleza.


“Tunawashtaki kwa BMT (Baraza la Michezo la Tanzania) na baadaye tunaweza hata kuwafikisha mahakamani,” alisema daktari huyo wa zamani wa Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic