September 16, 2014

 Real Madrid imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Basel ya Uswiss katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa ndani ya Santiago Bernabeu.


Gareth Bale, Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na James Rodrigues walikuwa kati ya waliochangia mabao hayo matano.

Liverpool nayo ikiwa imerejea tena kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuikosa kitambo, ilifanikiwa kuibuka na ushindi.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ludogorets, Liverpool ikiwa nyumbani Anfield Mario Balotelli na nahodha Steven Gerrard aliyefunga mkwaju wa penalti katika dakika ya 90 ndiyo walikuwa mashujaa wa leo.
Lakini ilikuwa bahati mbaya kwa Arsenal iliyokuwa ugenini nchini Ujerumani dhidi ya Borussia Dortmund ambayo iliwapa kichapo cha mabao 2-0.

Waliowauwa Arsenal ni Ciro Immobile na Aubameyang na juhudi za vijana wa Wenger hazikufanikiwa angalau kupata bao la kufutia machozi.
Juventus wakiwa nyumbani, wakaifunga Malmo ya Sweden kwa mabao 2-0 na Benfika ikiwa nyumbani pia ikalala kwa mabao 2-0 dhidi ya Zenit.
Galatasaray ikiwa Istambul, ikashikiliwa kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Anderlecht ya  Ubelgiji. Monaco ya Ufaransa ikajitutumua kwa kuichapa Bayer Leverkusen kwa bao 1-0 lililofungwa  Joao Moutinho.
Olimpiako nayo ikawashangaza wengi, ikiwa nyumbani ikawachapa wabishi Atletico kwa mabao 3-2 katika mechi safi yenye ushindani mkubwa.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic