September 23, 2014

Hali imeonekana kuwa nzurio kutokana na Manchester United kuendelea kuboronga na safu yake ya ulinzi kuwa nyanya.

Mechi iliyopita Man United imefungwa mabao 5-3 na Leicester City ikiwa ni bada ya kuongeza kwa mabao 3-1.
Picha unayoiona, inaonyesha kiasi gani safu yake ya ulinzi inacheza shaghalabagala. Wachezaji hawakai katika sehemu zao.
Angalia aliyewekewa namba 2, huyo ni Blackett ambaye ameamua kubaki nyuma peke yake bila ya kuangalia wenzake wamejipanga vipi.
Ukiachana na hivyo, katika picha hiyo kuna wachezaji saba wa Man United na watatu tu wa Leicester City lakini bado waliweza kuleta madhara.
Kitu kikubwa cha tatu, katika wachezaji saba wa Man United, hakuna hata mmoja aliyemkaba mchezaji mmoja tu kati ya watatu wa Leicester City.
Hayo ndiyo sehemu ya madudu ya safu ya ulinzi ya Man United.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic