September 20, 2014



Mtibwa Sugar chini ya Mecky Maxime imeifunga kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.
Yanga imelala ikiwa chini ya Marcio Maximo ambaye alikuwa mwalimu wa Maxime wakati akiinoa Taifa Stars.

Katika mechi hiyo leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku mashabiki wa Yanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi, timu yao ilitawala kipindi cha kwanza tu.
Lakini ikashindwa kuonyesha cheche katika kipindi cha pili na kulala kwa mabao 2-0.
Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 56 na dakika tatu baadaye Ame Ally akafunga la pili na kuimaliza Yanga.

Juhudi za Yanga kutaka kusawazisha hazikuzaa matunda na Mtibwa ndiyo walioonekana kukitawala kipindi cha pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic